Sheria na Masharti

Sheria na Masharti ya Matumizi – MindZetu
Tarehe ya Mwisho Kusasisha: March, 30 2026

Karibu kwenye MindZetu – blogi inayojikita katika kutoa maudhui ya fikra, maarifa, maendeleo binafsi, afya, elimu na uwekezaji. Kwa kuendelea kutumia blogi hii, unakubaliana na Sheria na Masharti yafuatayo. Tafadhali yasome kwa makini.

1. Matumizi Halali ya Tovuti
Unaruhusiwa kutumia MindZetu kwa madhumuni ya binafsi au kielimu tu. Hairuhusiwi:
Kuchapisha, kusambaza au kunukuu maudhui kwa matumizi ya kibiashara bila ruhusa ya maandishi ama Kuweka maudhui yenye lugha chafu, chuki, au yanayokiuka sheria za Tanzania. Kuwasilisha maoni yanayokiuka heshima au haki za watu wengine.

2. Haki Miliki (Copyright)
Maudhui yote (makala, picha, video, na sauti) yaliyopo kwenye blogi hii ni mali ya MindZetu isipokuwa kama yamenukuliwa kutoka vyanzo vingine (na kutolewa taarifa rasmi ya chanzo). Hairuhusiwi: Kunakili au kuiga maudhui bila kibali. Kutafsiri maudhui kwa lengo la kibiashara bila ruhusa.

3. Mauzo ya Bidhaa za Kidijitali
  • Malipo: Malipo yote yanafanyika kupitia mifumo salama (kama Selar). Bidhaa itatolewa tu baada ya malipo kukamilika.
  • Hakuna Kurudishiwa Pesa (No Refund Policy): Kwa sababu bidhaa za kidijitali (kama PDF, Presets, au Kozi) haziwezi kurudishwa zikishapakuliwa, hatutoi huduma ya kurudisha pesa (Refund). Tafadhali soma maelezo ya bidhaa kwa umakini kabla ya kununua.
  • Matumizi ya Binafsi: Bidhaa unazonunua ni kwa ajili ya matumizi yako binafsi pekee. Huruhusiwi kuzigawa kwa watu wengine au kuziuza tena.

4. Usahihi wa Taarifa
Lengo la makala na bidhaa zetu ni kutoa elimu na mwongozo. Ingawa tunajitahidi kutoa taarifa sahihi na zenye tija, matokeo ya kutumia maarifa haya yanategemea juhudi za mtu binafsi. MindZetu haitoi dhamana (guarantee) ya mafanikio ya kifedha au kibiashara kwa kila mtumiaji.

5. Mabadiliko ya Huduma
Tuna haki ya kubadilisha bei za bidhaa, kuondoa makala, au kubadilisha vigezo hivi wakati wowote bila kutoa taarifa mapema. Ni jukumu la mtumiaji kupitia ukurasa huu mara kwa mara.

6. Sheria Inayotumika
Vigezo hivi vinaongozwa na sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Migogoro yoyote itatatuliwa kwa kufuata taratibu za kisheria za nchi.

7. Taarifa za Watumiaji
Tunachukua kwa uzito taarifa binafsi unazotoa (k.m. jina, barua pepe unapojisajili au kutoa maoni). Hatutaziuza wala kuzisambaza kwa mtu wa tatu isipokuwa kwa sababu za kisheria au kiusalama.

8. Viungo vya Nje (External Links)
Blogi hii inaweza kuwa na viungo kwenda kwenye tovuti au blogi nyingine. Hatutawajibika kwa maudhui, sera au usalama wa tovuti hizo.

9. Kanusho (Disclaimer)
Maoni yote yaliyotolewa kwenye blogi hii ni ya waandishi binafsi na hayawakilishi rasmi mtazamo wa MindZetu. Tunajaribu kutoa taarifa sahihi, lakini hatuhakikishi usahihi wake kwa asilimia 100.

10. Mabadiliko ya Masharti
MindZetu inaweza kubadili sheria na masharti haya wakati wowote bila kutoa taarifa ya moja kwa moja. Tunashauri utumie ukurasa huu mara kwa mara kusoma toleo jipya.

​Wasiliana Nasi

​Kama una swali au malalamiko yoyote kuhusu bidhaa au huduma zetu, tafadhali tuandikie kupitia:

  • Barua Pepe: barakakabanza0@gmail.com
  • WhatsApp: https://wa.me/message/FVGHEEPLPDT7I1

Chapisha Maoni

0 Maoni